Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Historia

Baraza la Vijana ni chombo kinachojitegemea kilichoanzishwa chini ya Sheria namba 16 ya mwaka 2013 ambayo imetiwa saini tarehe 30/06/2014 na aliekuwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Baraza la Vijana la Zanzibar limeundwa kwa mujibu wa matakwa ya kisera na kisheria yanayoelekeza haja ya kuwajenga vijana kuutambua utaifa wao, hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu. Pia kuifahamu kwa kina jamii, kiuchumi, hali halisi kiutamaduni na upeo wake; kufanya kazi kama jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar; na kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii na kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi.

Mambo Muhimu Yanayoeleza Uundaji wa Baraza

Katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 – 2015, mwezi wa Aprili, 2015, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alifanya uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza Zanzibar ambaye ndiye Mtendaji na Mratibu wa Sekretarieti ya Baraza la Vijana Taifa kwa mujibu wa Sheria ya Kuanzisha Baraza la Vijana Zanzibar.

Baada ya uteuzi wa Katibu Mtendaji, harakati na taratibu za uchaguzi kwa Mabaraza ya Vijana Kishehia, Wilaya na Kitaifa zikaanza. Mwezi Februari hadi Juni, 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa Mabaraza ya Vijana ngazi ya Shehia. Mwezi Juni hadi Julai 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi ngazi za Wilaya na mwezi Septemba 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi ngazi ya Taifa.

Baraza la Vijana Zanzibar lilifanya tena Uchaguzi wa mwaka 2021 na kuwapata viongozi wapya kama Sheria ya Kuanzisha Baraza la Vijana inavyoelekeza kufanya hivyo kila baada ya miaka mitatu.

Muundo

Malengo

Taarifa za Miradi