Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Mawasiliano - Baraza la Vijana Zanzibar

Kikao cha Baraza la Watendaji

News Image

Mwandishi: Bahati Habibu Peter

Tarehe: Tuesday, 10th June 2025

Baraza la Vijana Zanzibar leo limefanya kikao cha Baraza la Watendaji robo ya tatu ambapo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza la Vijana Zanzibar kwa kipindi cha Januari hadi Machi na muelekeo wa shughuli mpya kwa bajeti ya mwaka 2025/2026.

Aidha kikao hicho kimejadili na kupokea ripoti ya Utekelezaji wa Programu za Baraza la Vijana Zanzibar ikiwa ni pamoja na Kampeni ya Amani ni Tunu Vijana Tuienzi, Mobile Youth Space (MYS) na Youth Future Hub (YFH).

Kikao kiliongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Yunus Juma Ali na kilihudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la Watendaji na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan.

Taarifa za Miradi